– Mchango wako ni mhimu kwangu –
Gadi Sedekia
akiwa Longido, Arusha, Tanzania .
SHALOM!
Mimi naitwa Gadi sedekia, naishi Arusha,ni mdogo wa kuzaliwa na aliyekuwa mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania, marehemu Fanuel Sedekia, pia nami ni mwimbaji wa nyimbo za injili. ( Baadhi ya kazi zangu ziko youtube kwa jina la Gadi sedekia)nimewiwa kuja kwako kwa unyenyekevu mkubwa kuomba msaada wako wa hali na mali kama mtanzania kunichangia mchango wa kupandikizwa Figo.
Kwanza kabisa nlipata tatizo la sukari ya utotoni ambapo kwa miaka 16 nimekuwa nikiishi kwa kuchoma sindano za insulin mara mbili kwa kutwa asubuhi na jioni
Kwa sasa nlipata tatizo la presha na kupata dalili za Figo kushindwa kufanya kazi vizuri, baadae Figo zilishindwa kabisa kufanya kazi ndipo nilipoanza kupata huduma ya kusafisha damu (Hemodialysis)

– Kutoa ni moyo, si utajiri –
Gadi Sedekia
akiwa kwenye mashine ya kuchuja sumu
Mungu ni mwema ana njia nyingi za uponyaji, nimepata msamaria wa kunipa figo, natakiwa kupata kiasi Cha zaidi ya milion 50 za kitanzania kuweza kupandikizwa hiyo Figo, ndio maana nmekuja kwako mdogo wako niweze kupata msaada wa kupata hicho kiasi.
ukweli mateso ni makali sana, kama kijana pia bado Niko na ndoto nyingi sana
nakuomba msaada wako niweze kurudisha tabasamu langu la kiafya ambalo limepotea haswa kwa muda wote huo nategemea dialysis maana hata uwezo wa kukojoa hata tone

– kupumua kwa shida –
Sumu inapozidi
unapumua kwa shida na unahitaji hewa safi
Mgonjwa wa figo anaweza kujisikia mchovu kupita kiasi, kuvimba mwili (hasa miguu, uso, na mikono), kuwa na shida ya kupumua, na kukojoa mara kwa mara hasa usiku. Dalili hizi huashiria kuwa figo haziwezi kufanya kazi zake ipasavyo.
Kichwa kuuma au kizunguzungu kutokana na shinikizo la damu au sumu mwilini
• Kupoteza hamu ya kula, kichefuchefu au kutapika
• Maumivu ya kifua, hasa kama kuna maji kuzunguka mapafu

-zijue dalili za ugonjwa –
Mateso ni Makali
Chache hizi ni dalili za shida ya figo;
• Kupungua kwa kiasi cha mkojo au kukojoa mara kwa mara hasa usiku
• Uvimbishaji wa miguu, uso, macho, na mikono
• Kuchoka kupita kiasi (fatigue) hata bila kufanya kazi ngumu
• Kupumua kwa shida au kuhisi kama unakosa hewa
• Kuwashwa mwili mzima bila sababu ya wazi
• Mkojo kuwa na damu au povu nyingi
• Kupoteza hamu ya kula, kichefuchefu au kutapika
• Maumivu ya kifua, hasa kama kuna maji kuzunguka mapafu
• Mwili kupata michubuko kwa urahisi
Kichwa kuuma au kizunguzungu kutokana na shinikizo la damu au sumu mwilini


Kazi ya Maabara Hospitalini
Hii ni kazi ya utaalam wa maabara hospitalini ambayo Gadi ni mtaalam na aliisomea.
